Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo aishika mkono Iringa DC
Na Ummi Mohamed (Afisa habari na Uhusiano,Iringa –DC)
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Bw.Gerald Kusaya amewaagiza Maafisa Umwagiliaji kutoka ofisini kwake kwenda kuongeza kasi ya ujenzi na upembuzi ya kinifu katika skimu za umwagiliaji zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Kauli hiyo ameitoa Septemba 4 alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Iringa na kuangalia uharibifu ulisababishwa na mvua zilizopita kiasi zilizonyesha katika msimu wa 2019/2020 katika Tarafa ya Idodi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Akisoma taarifa fupi ya kilimo,umwagiliaji na ushirika kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Afisa kilimo wa Wilaya Bi.Lucy Nyalu alisema katika skimu kumi na nne zilizoathiriwa na mvua hizo skimu ya Mkombozi,Mlenge, Magozi na Luganga zimeathiriwa zaidi na kupelekea mto kuhama katika njia yake ya asili na kwenda katika mashamba ya wakulima.
Alisema msimu wa 2019/2020 hali ya upatikanaji wa mbolea ilikuwa ya kuridhisha mbolea ya kupandia ya DAP nay a kukuzia UREA ziliuzwa kwa mfumo wa bei elekezi, kwa msimu wa 2019/2020 mahitaji ya mbolea kwa halmashauri ilikuwa tani 8,717 ambapo DAP tani 2,740,UREA tani 1,985,CANtani 1,250 NPK tani 2,586 na SA156.
Bw.Kusaya alipokea taarifa hiyo na kuahadi kutoa kiasi cha shiringi milioni 350 na wataalam katika Wizara yake ili kazi hiyo ya upembuzi yakinifu katika skimu ya Mkombozi iliyotengewa milioni mia moja ifanyike kwa haraka na ubora unaolingana na ferdha inayotolewa na serikali.
Aidha katika skimu ya Mlenge Bw.Kusaya ametoa fedha za ukarabati ambazo zote kwa pamoja zinafanya jumla ya milioni350 ambazo ameahidi kurudi baada ya wiki mbili ili kuangalia maelekezo yake kama yanatekelezwa ipasavyo.
“Kazi zote katika hizi skimu nne yaani Mkombozi,Mlenge,Magozi na Luganga zitaanza kufanyiwa ukarabati,matengenezo na upembuzi yakinifu Jumatatu ya 7Septemba mwaka huu wa 2020 ili wananchi hawa waweze kuendelea na shughuli za kilimo katika msimu wa mwaka huu 2020/2021 hasa kwa kuzingatia eneo hili lina asili ya ukame kwa kipindi kikubwa”alisema Kusaya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw.Bashir Muhoja ameishukuru Wizara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kupitia kwa Katibu Mkuu kwa kuona na kusikia kilio cha wakulima wanaotumia skimu hizo kwani kwa msimu wa 2019/2020 hawakupana mavuno mengi.
“Katibu Mkuu nakushukuru wewe na Wizara yako kwa kutuona na kutushika mkono sisi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kutupatia kiasi cha milioni 350 ili kuboresha na kuimarisha miundombinu ya skimu za umwagiliaji kama ulivyosikiam wakulima wangu wa Magozi wamevuna 2% tu kutokana na mvua kubwa za msimu 2019/2020 na kuharibu mashamba”alisema na kuongeza;
“Halmashauri itatoa walaam wake wote wa umwagiliaji na wengine watakaohitajika katika suala hili la uimarishaji na ukarabati wa skimu ili kazi ifanyike kwa ubora na kwa muda mfupi kama unavyoelekeza Katibu Mkuu”alisema Bw.Muhoja.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa