Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Afanya Ziara
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Bi. Mary Maganga amefanya ziara na kukagua mradi wa “Uarejeshaji Endelevu Mazingira na Uhifadhi wa Bayoanuai Tanzania, ambao unatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika Kata ya Nzihi Kijiji cha Ilalasimba, Februari 28, 2024.
Katika ziara hiyo Bi. Maganga huyo ameweza kujionea shughuli zilizotekelezwa katika Kijiji hicho ya kuhifadhi misitu ili kurejesha na kuhifadhi mazingira, pia amejionea vikundi mbalimbali zinazofanya shughuli zakuhifadhi mazingira na kuweka mashamba darasa na kufuga.
Katika kijiji hicho cha Ilalasimba kuna msitu wenye ukubwa wa Hekta 2,106.03 ambazo sawa na Ekari 5,204.11 zinazohifadhiwa kwa ajii ya kuboresha mazingira yaliyoharibiwa na tabianchi.
Kuna kikundi cha Israel ambacho kimeanzisha shamba darasa la mazao ya mahindi na maharage na wananchi wanaenda kujifunza hapo, kuna kikundi cha Agape nao wameweka shamba darasa la nyasi za kulisha mifugo, Kijiji cha Magubike ambako kuna msitu wa uliohifadhiwa.
Aidha, Bi. Maganga ameweza kufika hadi katika Kiwanda cha Virdium kinachotengeneza mkaa kwa kutumia nyasi, kwa lengo la kuhifadhi mazingira bila kukata miti.
Bi. Maganga ameongozana na Kamati Kuu ya Kuhifadhi Mazingira na kuridhishwa na mradi huo. Pia ameweza kutoa maelekezo kuwa, amesisitiza watendaji wawe wanaweka kumbukumbu sahihii za kimaandishi kwa hatua ya mradi (Documentation) ili vizazi vijavyo waweze kujifunza kupitia kumbukumbu hizo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, amemshukuru Bi. Maganga kwa ujio wake na kukagua shughuli za uhifadhi, na ameomba kuwezeshwa kuhifadhi msitu wa Milima ya Nyang’oro iliyopo Kata ya Nyang’oro ili waweze kuwa na uhifadhi enedelevu.
Bi. Maganga amewashukuru wajumbe na wananchi wa Kata ya Nzihi kwa kukubali kuhifadha shughuli za uhifadhi mazingira.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa