Kiasi cha Tsh. 89,697,923/- Kimetengwa Kwa Ajili ya Utekelezaji wa Afua za Lishe Kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
Bajeti hiyo ambayo imepangwa leo Novemba 29, 2023 ikiongozwa na Afisa Lishe wa Halmashauri Bi. Tiliza Mbulla, imebainisha kuwa kiasi cha Shilingi 63,837,923/- kutoka Mapato ya Ndani ya Halmashauri na Kiasi cha Shilingi 21,020,000/- ni Ruzuku kutoka Serikali Kuu, na kufanya jumla ya Bajeti hiyo kuwa Shilingi 89,697,923/-
Halmashauri imeendelea kupambana na matatizo ya lishe duni kwa makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo watoto wenye umri chini ya miaka mitano 47,158, kina mama wajawazito 12,908 kwa Mwaka wa Fedha 202/2023, pia hali ya lishe kwa makundi mengine ya wananchi wanaokadiriwa kuwa 322,704 kwa ujumla wao.
Aidha, shughuli za mapambano dhidi ya lishe duni zinafanyika kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa lishe kwa kuzingatia mikakati ya lishe na kufuata vipaumbele vilivyowekwa katika Mpango Jumuishi wa Taifa wa Lishe (NMNAP II 2021/2022 – 2025/2026).
Utekelezaji wa Afua za Lishe umekuwa na ufanisi kwa uratibu wa watoa huduma 268 wa ngazi ya jamii (CHWs) pamoja na watoa huduma wa afya katika vituo 81 vya kutolea huduma za afya.
Akibainisha vipaumbele vya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Afisa Lishe Bi. Avelina Selemani amesema “Lishe ya akina mama, watoto na vijana balehe, Lishe katika siku 1000 za kwanza, Utambuzi na matibabu ya utapiamlo wa kadri na mkali kwa watoto chini ya miaka mitano, Elimu ya kuzuia magonjwa yasiyoambukiza anayohusiana na lishe (DRNCD), Matumizi ya virutubishi vya nyongeza (Vitamin A.) na matibau ya minyoo na Uzalishaji na matumizi ya vyakula mchanganyiko (makundi 6 ya chakula”.
Aidha, Bi. Avelina ameweza kutaja changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa Afua za Lishe kuwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti hasa kwa Idara mtambuka, hivyo kufanya utekelezaji kwa uchache ikilinganishwa na mahitaji halisi. Ukosefu wa usafiri, mafuta na posho kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu wa shughuli za lishe, hivyo shughuli kukosa uendelevu.
Pamoja na changamoto hizo, Bi. Avelina ametoa njia ya kuweza kukabiliana nazo ikiwa ni kushirikisha Wadau ili kuweza kusaidia hasa katika suala la usafiri.
Ingawa kumekuwepo na changamoto hizo Wadau na jamii kwa ujumla bado wana uhitaji mkubwa wa elimu ya lishe kwani watu wengi wanaamini kuwa suala la lishe linawahusu watoto na wanawake tu.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa