ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA IRINGA KATA YA KIWELE, ULANDA NA NZIHI
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Kheri James amefanya ziara yake katika kata ya Kiwele, Ulanda na Nzihi mapema Mei 22, 2025.
Akiwa kata ya Kiwele Mhe. Kheri ametembelea ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Mfyome pamoja na miundombinu yake ambapo ametoa wito kwa mhandisi kuhakikisha kazi inakamilika mapema ndani ya siku saba ili wananchi waweze kupata huduma kwa uzuri kwani fedha imeshatolewa.
Baada ya hapo Mhe. Kheri amefanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Itagutwa kuongea na wananchi, kuhamasisha maeleo na kusikiliza na kutatua kero zao ambao ulitanguliwa na ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi.
Kata ya ulanda na Nzihi Mhe. Kheri amefaya mkutano wa hadhara kuongea na wananchi kisha kuweka jiwe la Msingi la uboreshaji wa skimu ya maji magubike.
#iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji
https://www.instagram.com/p/DKAjrOFsB4n/?igsh=MXM0ejdtc3BycDBrdA==
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa