Kikao cha Baraza la Wafanyakazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa chafanyika Januari 23, 2024 ambapo kimelenga kufanya mapitio ya Mpango wa Bajeti 2024/2025. Sanjari na hayo pia kumefanyika mapitio ya Bajeti ya 2022/2023 na 2023/2024 ambapo wajumbe wamejadili mambo kadhaa ikiwemo apendekezo ya vyanzo vya mapato.
Akizugumza wakati wa kikao Mhe. Mwenyekiti ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Dr. Marwa ametoa pongezi kwa wajumbe wa kikao kwa kushiriki na kutoa michango yao kwa umakini na kwamba michango yote imechukuliwa kwa ajili ya maamuzi mbalimbali.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa