“Kila Kata Wekeni Mikakati Maalum ya Kupunguza Hali Duni ya Lishe” – Mhe. Kheri James
Kikao cha Robo ya Tatu cha Tathmini ya Mkataba wa Hali ya Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, kimefanyika leo Mei 09, 2025 katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.
Moja kati ya maagizo katika kikao hicho ni kuwa Mhe. Kheri amewataka Watendaji wa Kata kuweka mikakati maalumu ya kupunguza hali duni ya lishe katika Kata zao kwa kutoa elimu kwa jamii hadi mashuleni.
Mhe. Kheri amesema pia, katika mikutano ya Kata kwa wananchi lazima iwepo agenda ya kudumu ya lishe, Vongozi wa Dini na Serikali waweze kutoa elimu kwa jamii juu ya umhimu wa lishe bora.
Kadhalika Mhe. Kheri amesisitiza kuwa watoto wajifunze namna ya kuandaa lishe bora wenyewe kwa kuwa wamejinza kutoka shuleni.
Hata hivyo Mhe. Kheri amewaonya Watendaji kuwa, kusiwepo na alama nyekundu ya kuonesha udhaifu wa lishe katika Kata yake, ikitokea basi Mtendaji huyo aandike barua mwenyewe ya kuchukuliwa hatua.
Mhe. Kheri amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kwa kufanya vizuri katika masuala ya usafi na kuifanya Halmashauri kushika nafasi ya Pili Kitaifa, na pia amepongeza kwa kusimamia miradi vizuri na kufanya Mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kufurahia miradi iliyokagaliwa na kufunguliwa.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Stephen Mhapa amewaambia Watendaji wa Kata kuwa, “endeleeni kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Mhe. Mkuu wa Wilaya hasa kwenye suala la muda. Kwamba mmepewa nafasi hizi kwa Imani hivyo mkafanye kazi kwa uaminifu. Pia tuendelee kushirikiana kutafuta masoko kwa wananchi wanaofanya shughuli za kiuchumi ili wasikate tamaa katika kutafuta kipato”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Robert Msunya amepokea pongezi zilizotolewa na Mkuu wa Wilaya na kuahidi kutoa msukumo katika masuala ya lishe, kwani watu wote ni Wadau wa Lishe.
Taasisi mbalimbali zikiwemo za World Vision na Assisting Small Farmers (ASF) wameendelea kutoa ushirikiano kwa kuanzisha vitalu na bustani za mbogomboga katika shule, ili kuendeleza suala la lishe kwa wanafunzi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa