Komred Mohamed Aboud Mohamed Afanya Ziara Mkoani Iringa
Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Komredi Mohamed Aboud Mohamed amefanya ziara Mkoani humo Oktoba 09, 2023.
Lengo la ziara ni kutambulishwa kuwa kama Mlezi wa Chama Mkoani Iringa, na kuangalia uhai wa Chama.
Akiongea katika hotuba zake maeneo mbalimbali aliyotembelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Komreid Aboud amesema, “yupo kukamilisha Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambazo ziliainishwa mwaka 2020. Kutokana na kutekeleza wa Ilani ya Chama, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, hivyo sisi tuna wajibu wa kumlipa kwa kumuombea dua na kumpigia kura nyingi wakati wa uchaguzi utakapofika”.
Komredi Aboud ameendelea kusema kuwa, “matatizo yote niliyosikia katika maeneo niliyotembelea nitayafanyika kazi kwa kuanza kuagiza viongozi wa Chama wa eneo husika ili waweze kuyatatua kwa haraka, ikiwemo maji, kadi za chama, barabara n.k.”.
Aidha, Komredi Aboud ameweza kutembelea Kituo cha Afya Kiwele, mkutano wa hadhara kijiji cha Mgera kwa Mjumbe wa Shina Namba 6, (Kata ya Kiwele), kikundi cha Ushonaji cha Binti Salha Foundation kilichopo Shule ya Sekondari William Lukuvi, Mkutano wa hadhara kwa Mjumbe wa Shina Namba 01, (Kata ya Ilolo Mpya), Hospitali ya Wilaya iliyopo Kijiji cha Mbuyuni Kitongoji cha Igodikafu (Kata ya Itunundu).
Katika ziara hiyo Komredi Aboud aliweza kuambatana na Wajumbe mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi Wilaya na Mkoa akiwemo MNEC Richard Kasesela, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Komredi Daud Yasin Mlowe na Wajumbe wengine.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa