M-MAMA YAJA MKOANI IRINGA
Mhe. Peres Boniphace Magiri Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa amezindua Mfumo wa Kidigitali wa huduma kwa akinamama wajawazito na watoto hasa katika eneo la usafirishaji na ufuatiliaji (M-MAMA) katika Mkoa wa Iringa, mpango utakaosaidia kuokoa maisha ya akinamama wajawazito na watoto wachanga kwa kuchelewa kupata huduma.
Akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa mpango huu Mhe. Magiri amesema, “M-Mama inakuja ili kuongeza thamani ya jitihada za Serikali hivyo, Mkoa wa Iringa tuna wajibu wa kulibeba jambo hili litapoanza 15.08.2023 kuhakikisha kuwa tunapunguza au kuondoa kabisa vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga”
Pia Mhe. Magiri ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuzindua rasmi mpango wa usafirishaji wa dharura wa akinamama wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga (M-Mama) Kitaifa Mkoani Dodoma, mpango ambao utasaidia kupunguza vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga utakaotekelezwa nchi nzima.
Naye Dr. Mshana Dastan kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi amesema Serikali imefanya jitihada za kununua magari ya kubebea wagonjwa (ambulance) Zaidi ya 700 ambapo kila Mkoa utapata gari ya Ambulance ya kisasa kabisa yenye huduma zote ndani za kitabibu na kila Halmashauri itapata gari mbili za Ambulance za kawaida mgao ambao utaenda kwa awamu. Sanjari na hayo pia Dr. Mshana amesema kuwa Ambulance zinapaswa kutumika kwa ajili ya kazi tarajiwa tu ambayo ni kuwahudumia wagonjwa na kufanya ukarabati wa zile zinazoharibika.
Kwa upande wake Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto (RRCHCO) Mkoa wa Iringa, Bi Wende Mwavika ameeleza hali halisi ya miundombinu na vifo vya wamama wajawazito na watoto vinavyotokea kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa sanjari na jitihada au hatua zinazochukuliwa kukabiliana na changamoto zilizojitokeza.
Kwa niaba ya Wenyeviti wa Halmashauri Mkoa wa Iringa Mhe. Stephen Mhapa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ameshukuru na kupongeza kuhusu mpango huu wa M-Mama ambao umeanza hatua ya awali kwa kuwashirikisha viongozi wanaowafikia wanchi moja kwa moja na kuomba ushirikishwaji huu uwe endelevu ili kuwa na uelewa wa pamoja hivyo kuleta ufanisi.
Mpango wa M-Mama utatumia kanzidata ya mawasiliano na kanzidata ya usimamizi na ufuatiliaji. Kutakuwa na kituo ngazi ya Mkoa ambacho kitakuwa ndio kituo cha kuratibu dharura (Dispatchers) na kituo kitakuwa kinapokea taarifa kutoka kwa wahudumu wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi mbalimbali na kuratibu masuala ya usafiri na ufuatiliaji wa huduma kwa mgonjwa. Namba itakayotumika kutolea taarifa ya dharura ni 115 ambayo ni tall free na itawafikia Dispatchers moja kwa moja kwa hatua.
Kwa mkoa wa Iringa Mpango huu unatarajiwa kuanza rasmi katikati ya mwezi August 2023 baada ya hatua zingine kufikiwa kulingana na mpango kazi ulioandaliwa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa