Maadhimisho ya Siku ya Lishe Duniani Yafanyika
Kila mwaka Oktoba 29 Dunia inaadhimisha Siku ya Lishe, na kwamba kila Mtanzania anapaswa kushiriki katika Maadhimisho hayo ili aweze kupata ujumbe utakaotolewa kwa Mwaka huo.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imeadhimisha siku hiyo Oktoba 30, katika Kata ya Mseke Kijiji cha Tanangozi na Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Diwani wa Kata ya Mseke Mhe. Mansour Mbaraka.
Akitoa hotuba yake Mhe. Mansour amesema, “Sasa ni wakati wa kutafakari kwa kina juu ya suala zima la lishe, kwani katika kipindi hiki ni muhimu kuzingatia afya ya vijana na kuwasaidia wazee kudumisha nguvu zao. Pia watoto walio chini ya miaka mitano wanahitaji lishe na virutubisho bora, kadhalika lishe bora kwa wanafunzi wawapo shuleni ni muhimu sana.”
Mhe. Masour ameendelea kusema kuwa, kwa wamama wajawazito wanatakiwa kupatiwa lishe ili imsaidie mtoto aliyepo tumboni. Napenda kutoa wito kwa jamii ni wajibu wetu kudumisha lishe kwenye familia zetu, kwani Lishe Bora ni Msingi kwa Maisha Bora”.
Naye mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Tiliza Mbula amesema, “tunatakiwa kufuata mwongozo wa ulaji wa chakula ambao ulizinduliwa Oktoba 2023, ambao kunatakiwa kuwepo na makundi sita ya vyakula kama; Protini, Mbogamboga, Mafuta, Madini, Wanga na Matunda, na kwamba vyakula hivi vinasaidia sana ukuaji wa mtoto.
Kauli Mbiu ya Mwaka Huu ni “Mchongo ni Afya Yako, Zingatia Unachokula”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa