Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Peter Serukamba akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Kamati ya Mwenge Mkoa, na Kamati ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wamefanya ziara kutembelea miradi ambayo Mwenge wa Uhuru utapita na kukagua miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Ziara hiyo imefanyika Aprili 08, 2025, kukagua miradi ambayo ni kwa ajili mapokezi ya Mwenge ni pamoja na Kata Migoli Kijiji cha Makatapola na kukagua majengo ya Shule ya Sekondari Mpya ya Makatapola.
Kamati imetembelea kwenye mradi wa barabara wa barabara ya kilomita 3 iliyopo katika kijiji cha Mbuyuni kuelekea Kata ya Izazi, kisha mradi wa jengo la jiko la kisasa katika Shule ya Sekondari Pawaga.
Kadhalika Kamati imetembelea Kata ya Kiwele Kijiji cha Mfyome katika ujenzi wa bwawa la samaki ambapo ni mradi wa vijana waliokopeshwa fedha za asilimia kumi.
Kamati imefika hadi eneo la makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Wilaya kijiji cha
Kamati imeendelea kusisitiza ubora wa kazi na kuendana na muda wa ukamilishaji miradi hiyo, ili kukidhi vigezo vya matakwa ya Mwenge.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa