Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James akagua miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2025.
Katika hatua ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa uhuru Mhe. Kheri James atembelea na kukagua miradi inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Iringa DC mapema Machi 28, 2025 sanjari na shughuli mbalimbali za vikundi.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni; ujenzi wa shule mpya ya sekondari Makatapola, ujenzi wa chumba cha darasa katika kata ya Mboliboli, ujenzi wa Godauni Mboliboli, ujenzi wa nyumba 3 za watumishi wa afyaza (3 in 1) zinazochukuwa familia 9, mradi wa barabara ya lami katika kijiji cha Mbuyuni, mradi wa majiko banifu shule ya sekondari Pawaga, na mradi wa maji kijiji cha Itagutwa kata ya Kiwele.
Vile vile kuna shughuli za ujasiriamali zinazofanywa na vijana kupitia vikundi vinavyonufaika na mkopo wa 10%, Klabu mbalimbali za wanafunzi na shughuli zingine za kijamii zinazofanywa na wananchi.
Mwenge wa Uhuru 2025 katika Halmashauri ya Wilaya unatarajiwa kupokelewa April 28, 2025 ukitokea Mkoani Dodoma ambapo unapambwa na kauli mbiu ifuatayo; “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa