Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano, Iringa -DC
Home boys yaibuka kidedea Punda Cup.
Timu ya mpira wa miguu ya Home boys kutoka Migoli imetwaa ubigwa wa Punda Cup 2020 baala ya kuichalaza bao 3 -0 timu ya Mtaa wa kati mwishoni mwa wiki, mashindano hayo ya yamedhaminiwa na INADES Formation Tanzania.
Fainali za mashindano hayo zilifanyika 18 Septemba 2020 katika viwanja vya stendi Migori ambapo dakika ya 2 ya kipindi cha kwanza mchezaji Salum Mawio alitikisa nyavu kwa bao la kwanza,na dakika ya nane nyavu za Mtaa wa kati zilitikiswa tena na mchazaji Robert Katunga katika kipindi cha kwanza.
Akizungumzia mchezo huo Afisa Mifugo na Uvuvi aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali hizo alisema Mechi zote za nusu fainali zilichenzwa kwa ustadi mkubwa huku nidhamu ikitawala kwa wachezaji wote wa hizo na kuonyesha kulizika na matokeo.
“kama Wachezaji wangekuwa hawakulizishwa na matokeo kungekuwa na malalamiko lakini timu zote zilibakia katika eneo hilo hadi mechi ya pili ya kumtafuta mshindi ilipo malizika na kupokea zawadi,kupiga picha ya Pamoja na kuondoka kwa nidhamu bila kutumia lugha za matusi wala vitisho miongoni mwa muamuzi ama mtangazaji”alisema.
Magoli hayo lifungwa na Salumu Mawio ambaye kipindi cha pili alifanikiwa kupachika tena bao la tatu kwa timu yake ya Home boys dhidi ya Mtaa wa kati.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa