Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewataka Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhakikisha wanaisimamia miradi yote iliyopo kwenye Kata zao
Ameyasema hayo leo Mei 28. 2024 wakati aliposhiriki katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa lililofanyika kwenye Ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Akizungumza na Madiwani hao Mhe. Serukamba amesema kuwa, miradi mingi kwenye Halmashauri bado haijakamilika na hii ni kutokana na kukosekana kwa usimamizi wa miradi hiyo, hivyo amewataka Madiwani kuhakikisha wanasimamia kwa nguvu zao zote na kuachana na visingizio vya kusema kuwa Wataalamu ndio wanaopaswa kusimamia miradi hiyo.
"Mkurugenzi Madiwani wote hawa ni wa kwako, wote watume wakasimamie kazi za miradi iishe kwa wakati, Ndugu Madiwani hakikisheni mnasimamia miradi inakamilika kwa wakati".
Pia Mhe. Serukamba ameongeza kwa kutoa rai kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha pindi fedha za miradi zinapofika ziende moja kwa moja kwenye miradi na zisikae Halmashauri. Ili miradi iweze kukamilika kwa wakati.
Kwa upande mwingine Mhe. Serukamba ameendelea kuwahimiza Madiwani hao kuwa na umoja na mshikamano katika kuisongesha mbele halmashauri hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa Stephen Mhapa kwa niaba ya Madiwani, amepokea maagizo yote na ameahidi watayafanyia kazi.
Mhe. Mhapa ameinheza kusema kuwa, anahitaji hoja zote zinazotolewa na wajumbe zijibiwe na Wenyeviti wa Kamati.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa