Mafunzo kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura yamefunguliwa leo Desemba 23, 2024 katika kituo cha Migoli shule ya sekondari Nyerere na Ipamba katika shule ya sekondari Tosamaganga.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Afisa Mwandikishaji Bi. Beatrice Augustino amesema, mafunzo haya yana lengo la kuwapa wahusika ujuzi hivyo watumie vema ujuzi watakaoupata ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi
Aidha Bi. Beatrice ametoa wito kwa washiriki wote kutunza vifaa watakavyokabidhiwa kwa kazi husika sanjari na kufuata maelekezo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi ili kazi iweze kufanyika kwa usahihi hapo zoezi litakapoanza.
“Ninatoa wito kwenu kuhakikisha mnavitunza vifaa vyote vitakavyotumika katika uboreshaji na kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili muweze kufanyia kazi kwa usahihi wakati zoezi litakapokuwa linaendelea", Amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndugu Robert Masunya amesisitiza usikivu kwa washiriki wa mafunzo ili waweze kujifunza kwani kila hatuanina miongozo yake na kuwasisitiza washiriki kutunza viapo vyao kwa kufanya mambo yanayowahusu tu na kuachana na mambo mengine yasiyowahusu kwa kila mtu kutimiza wajibu wake
Katika mafunzo haya ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, maafisa waadikishaji wasaidizi na waendeshaji wa vifaa vya BVR wanaendelea kupatiwa mafuzo katika vituo vyote viwili vilivyoko jimbo la Kalenga na Ismani ambayo yameanza Desemba 23, 2024 na kuhitimishwa Desemba 24, 2024.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa