Mafunzo ya Kupima Utendaji Kazi (OPRAS) Yafanyika
Novemba 21, 2023 yamefanyika mafunzo ya kupima utendaji kazi (OPRAS), ambao utafanya kutoka katika mtindo wa zamani wa kujaza kwenye makaratasi na kuhamia kidigitali zaidi.
Akitoa utangulizi wa namna ya ufanyikaji wa mfumo huo muwezeshaji Bi. Mariamu Mussa kutoka Ofisi ya Rais Utumishi amesema, “mfumo huu unatuhamisha kutoka katika uzamani na kwenda kisasa zaidi kwa kujaza na kupima utendaji kazi wa mtumishi kwa urahisi zaidi.
Njia hii inasaidia kutotumia zaidi makaratasi na badala yake tunatumia njia ya mtandao tu, kazi zinazofanywa na mtumishi yeyote kuonekana hadi ngazi za juu kuanzia zile za siku hadi za mwaka mzima, na kufanya mpimaji kupima kwa urahisi.”
Mafunzo hayo yamenza kufanyika kwa Wakuu wa Idara na Vitengo na kufuatiwa na Watumishi wengine wote. Mafunzo yataendelea hadi Novemba 24, 2023 kwa Watumishi waliopo kwenye Kata mbalimbali za Halmashauri.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa