Watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa hasa wale wa ngazi ya usimamizi wapatiwa mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa mtumishi (Emmployee Self Service – ESS) Juni 25, 2025 katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Madirisha ya huduma yaliyoangaziwa ni; e-utendaji, e-uhamisho, e-mkopo, e-likizo, e-wekeza, na salary slip. Mafunzo haya yametolewa mahususi kwa ajili ya watumishi waliopo kwenye ngazi ya usimamizi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri kuanzia makao makuu hadi ngazi za msingi za utendaji kazi.
Msisitizo wa mafunzo hay ani kukumbushana kuhusiana na mfumo mzima wa e-utendaji hususani kwenye kipengele cha tathmini ya utendaji wa watumishi kipengele ambacho kisipozingatiwa kinashusha alama za utendaji za mtumishi na kupelekea changamoto ya upandaji wa madaraja.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa