Mafuriko Migoli - DC Kessy Aongoza Kutoa Mkono wa Pole
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Veronica Kessy Desemba 06, 2023 ameongoza kwenda Migoli kutoa mkono wa pole kwa wananchi wahanga wa janga la mafuriko, Kijiji cha Migoli Kata ya Migoli.
Mafuriko hayo yalitokea Desemba 05, 2023 na kusababisha baadhi ya kaya kukosa mahala pa kuishi na kukosa chakula.
Pole hiyo ni pamoja na unga, maharage na sukari.
Mheshimiwa Kessy anomba wadau na wananchi mbalimbali kumuunga mkono kwa kwenda kutoa pole kwa wananchi hao wahanga wa mafuriko.
Mtaa wa Gangilonga
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0767778106
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa