Mamlaka ya Mawasilano Tanzania (TCRA) Nyanda za Juu Kusini yatoa mafunzo kwa Watumishi wa Umma jinsi ya kutumia mitandao mbalimbali
Mamlaka ya hiyo imetoa mafunzo hayo jana katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikijumuisha Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Taasisi za simu (Vodacom, Tigo, Halotel na Airtel).
Akitoa salamu katika mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu Ndugu Deogratius Yinza amesema, “Sasa hivi Dunia inaenda kimtandao zaidi hasa kwa shughuli mbalimbali, hivyo tujitahidi kutumia fursa hizi za mtandao kwa manufaa yetu. Japo zipo changamoto nyingi kama utapeli kwenye simu, unyanyasaji, maudhui yasiyofaa kama picha za utupu, taarifa za uongo ushawishi mbalimbali na mengine mengi, inatupasa kujihadhari sana”.
Ndugu Yinza ameongeza kusema kuwa, kutuma nyaraka mbalimbali za Serikali kwenye mitandao siyo sawa, ni kosa kisheria, hasa zikiwa nyaraka za siri. Sekta ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ipo kisheria na ni Taasisi ya Serikali ina Taratibu na Miongozo yake.
Pia amewashukuru Watumishi wote waliohudhuria mafunzo haya na kuomba kuendelea kutumia mitandao kwa kujihadhari na matumizi sahihi.
Naye Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Nyanda za Juu Kusini Ndugu Asajile John Mwakisisile amesema, ‘Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni Taasisi ya Serikali ambayo ilianzishwa mwaka 2003, ambapo inasimamia mawasiliano nchini’.
Pia Mamlaka hii inashirikiana na Mitandao ya Simu mbalimbali ambayo ipo nchini kote, na kushughulikia mambo mbalimbali yanayohusu matumizi ya simu, pia kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa watumiaji. Aidha, inatoa nafasi kwa watumiaji wa mitandao kutoa malalamiko yao na kuhakikisha yanashughulikiwa.
Serikali kupitia Sekta ya Mawasiliano inapata kodi yake kutoka kwenye vyombo vya simu. Hivyo Mamlaka in jukumu la kusimami watoa huduma na wanaohudumiwa katika suala zima la mawasiliano bila kuwaumiza watoa huduma na wapokeaji huduma.
Pamoja na maelezo mengi ya kazi za Mamlaka na Mawasilaino, Meneje alitoa nafasi ya kuuliza maswali, na maswali mbalimbali yaliulizwa na kujibiwa ipasavyo.
“Nina Imani baada ya mafunzo haya mtakuwa mabalozi wazuri kwa wananchi huko mtaani, kwa kuwaelekeza matumizi sahihi ya mitandao ya simu”, haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Mohamed Moyo alipokuwa anafunga mafunzo haya na kusisitiza watumishi wawe wanafanya matumizi sahihi ya mitandao.
Pia Mh. Moyo amewaomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuleta mitandao (minara) ya simu katika Vijiji ambayo bado mawasiliano ni ya shida, na kufafanua baadhi ya Kata ambazo hazina mitandao kama Malengamakali, Kihanga, Nyang’oro, Masaka na kwingineko, ili wananchi waweze kunufaika na mawasiliano.
“Kuna faida kubwa sana kwa kupata mitandao, wanaanchi wanaweza kufanya biashara kupitia simu na kufanya shughuli zao kidigitali zaidi”, amesema Mh. Moyo.
Pia Mh. Moyo ameowaomba Mamlaka kuboresha miundombunu ya simu upande wa mtandao (networks), ili mtu afanye mawasiliano ya uhakika, kadhalika upande wa kupakua (downloads) vitu mbalimbali.
Mwisho amewashukuru Watumishi kushiriki mafunzo hayo kwa wingi na kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliyojifunza na maswali ambayo walikuwa wanajiuliza.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa