Mashindano ya MBOMIPA Yahitimishwa
Matumizi Bora ya Maliasaili Idodi na Pawaga (MBOMIPA), wameendelea kutoa elimu katika Jumuiya za Uhifadhi, ili kulinda mazingira na maliasili kwa ujumla.
Katika kushirikiana na jamii MBOMIPA iliandaa mashindano ya mpira wa miguu kwa Tarafa ya Pawaga na Idodi ili kuleta uelewa wa pamoja katika jambo la uhifadhi mazingira, ambapo mashindano hayo yalianza Agosti 20, 2023 na kuhitimishwa Septemba 05/2023, na kufanikiwa kupata washindi katika mashindano hayo.
Akitoa hotuba yake katika kufunga mashindano hayo Mgeni Rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa amesema, “anawashukuru waandaaji wa mashindano haya kwani yameleta tija kwa kuleta jamii pamoja, pia kuona vipaji walivyonavyo vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa”.
Mheshimiwa Mhapa ameomba mashindano haya yafanyike tena mwakani kwani yanahamasisha vijana na kuwatoa katika mambo ya ujangiri, badala yake wanajiwekeza katika kulinda rasilimali zao.
Pamoja na kufunga mashindano hayo Mheshimiwa Mhapa aliweza kukabidhi zawadi kwa washindi mbalimbali ambao walipatikana.
Golikipa Bora toka Kijiji cha Tungamalenga Kata ya Idodi amepata zawadi ya mpira wenye thamani ya Shilinh 40,000/-, Mfungaji Bora Milton Luhego kutoka Kijiji cha Mahuninga Kata ya Mahuninga amepata zawadi ya mpira wenye thamani ya Shilingi 40,000/-, Mchezaji Bora Selemani Mbwawa kutoka Kijiji cha Kinyika Kata ya Mlenge amepata zawadi ya mpira wenye thamani ya Shilingi 40,000/-
Kadhalika zawadi imetolewa kwa Shule ya Sekondari Pawaga kwa kutoa uwanja utumike katika fainali za mashindano hayo, kwa kupata mpira wenye thamani ya Shilingi 40,000/-
Mshindi wa Nne ambao ni Mboliboli FC wamepata zawadi ya Tshirts, ambapo Robo fainali za mchezo huo ulikuwa kati ya Makifu FC kutoka Kata ya Mahuninga, Luganga FC kutoka Kata ya Ilolompya, Mbuyuni FC kutoka Kata ya Itunundu na Malinzanga FC kutoka Kata ya Mlowa.
Mshindi wa Tatu ni Mahuninga FC wamepata zawadi ya Shilingi 500,000/=, Mshindi wa Pili ni Tungamalenga FC wamepata zawadi ya Shilingi 700,000/=.
Hatimaye Kinyika FC wameibuka kuwa Mshindi wa Kwanza kwa Mashindano ya Kombe la MBOMIPA na kupata zawadi ya Shilingi 1,000,000/- na Kombe (Ngao) kutoka Kata ya Mlenge Tarafa ya Pawaga kwa mwaka 2023.
Mashindano haya yaliandaliwa na kudhaminiwa na Mashirika ya Lion Landscap kwa kushirikiana na Southern Tanzania Elephant Program – STEP.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa