MATIBABU YA VIKOPE (TRAKOMA) YATOLEWA KWENYE HOSPITALI YA WILAYA YA IRINGA- IGODIKAFU
Wataalamu wa macho kutoka Wizara ya afya, na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kushirikiana na wadau kutoka shirika lisilo la kiserikali la Helen Keller International wamefika kwenye hospitali ya Wilaya ya Iringa (Igodikafu) tarehe10.08.2023 kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa wa Vikope (Trakoma), matibabu ambayo yanatolewa bila malipo kwa wote wenye changamoto hiyo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, mwakilishi kutoka Wizara ya Afya kwa upande wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaombele ndg Husein Kilwanile amesema, “Wizara imekuja na utaratibu mpya kwa kushirikiana na WHO wa kutafuta wagonjwa nyumba kwa nyumba ili kuwafikia wote wenye tatizo la vikope na kuwahudumia”
Naye Mtaalamu wa matibabu ya macho Dr. Roida Augustino amesema, “Mafunzo yametolewa kwa wahudumu ambapo hadi sasa kata 19 zimefikiwa kati ya kata 28 za Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na matibabu kwa wagojwa yamefanyika kwa kata 16 ambapo wagonjwa wapatao 179 wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri”
Kwa upande wao jamii na wananchi waliofikiwa na huduma hii wameipogeza sana serikali kupitia Wizara ya Afya, Halmasahuri ya Wilaya ya Iringa na Wadau kutoka shirika la Helen Keller Internation kwa kuwezesha huduma hii kuwafikia watu hadi ngazi ya jamii ambapo inaondoa kabisa gharama za matibabu ya ugonjwa huo kama wagonjwa wangefuata huduma hii kwenye hospitali kubwa.
Shirika la Helen Keller Internation limeweza kuisaidia hospitali ya Wilaya ya Iringa - Igodikafu kumsomesha course ya macho za awali muuguzi mmoja na kwamba clinic ya macho imefunguliwa ambapo mwanzoni haikuwepo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa