• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe Za Watumishi |
Iringa District Council
Iringa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu sekondari
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo umwagiliaji na ushirika
      • Mazingira na Usafishaji
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA NA Uhusiano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipango,Utawala na Uchumi
      • UKIMWI
      • Afya Elimu na Maji
      • UMazingira, uchumi na Ujenzi
      • Maadili
    • Ratiba Ya Vikao mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Hudumakwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video za Shughuli Mbalimbali za kiofisi na za Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MBOMIPA Kung'ara Tena

Imewekwa : August 21st, 2023

MBOMIPA Kung’ara Tena

Elimu imeendelea kutolewa juu ya Uhifadhi wa Matumizi Bora ya Maliasili kwa Idodi na Pawaga (MBOMIPA) na Maeneo ya Jamii ya Hifadhi ya Wanyamapori (Wildlife Management Area – WMA) kwenye vijiji vinavyozunguka Mbuga ya Wanyama ya Ruaha, ambapo Wadau wa Mashirika ya Lion Landscape na STEPS wameweza kutoa elimu hiyo kuanzia shule za Msingi na Sekondari katika vijiji vya Tarafa ya Pawaga na Idodi na kushindanisha michezo ya mpira wa miguu kwa timu mbalimbali za vijiji.

Sambamba na utoaji elimu kwa wanafunzi pia wameweza kutoa elimu kwa jamii kwa kuanzisha mashindano ya michezo kwa kugombea zawadi na Makombe ikiwa ni njia nyingine ya kutoa elimu, ambapo ufunguzi umefanyika tarehe 20/08/2023 katika Kata ya Mlolo Kijiji cha Malinzanga.

Akiongea katika ufunguzi wa mashindano hayo Mkuu wa Kitengo cha Maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Fatuma Juma amesema, “pamoja na kutoa elimu juu ya uhifadhi wa maliasili na mazingira, pia michezo ni afya. Michezo hii inahamasisha jamii kushirikiana na kujenga uelewa wa pamoja juu ya uhifadhi”.

Akiongea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mratibu wa Mashindano hayo Ndugu Wiston Mtandamo amesema, “mashindano haya yanachochea uelewa wa namna ya kuishi na wanyama pori ambao ni rasilimali za Taifa letu. Pia inaongea uelewa wa kuepukana na mambo ya ujangiri katika kuwawinda au kuwaua wanyama pori na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla”.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Maliasili na Wanyamapori Ndugu Jonas Mkusa amesema, “nawapongeza Wadau wa MBOMIPA kwa kuanzisha mashindano haya na kwamba hii itachochea umuhimu wa uhifadhi katika jamii, na kutokomeza shughuli za ujangiri na uwindaji haramu”.

Mechi ya ufunguzi ilikuwa kati ya timu ya Malinzanga ya Kata ya Mlowa Kijiji cha Mlowa na timu ya Magombwe ya Kata ya Mlenge Kijiji cha Magombwe, ambapo mshindi alipatikana timu ya Magombwe kwa mikwaju ya penati.

Matangazo

  • PONGEZI June 24, 2025
  • KUITWA KWENYE USAHILI WA UBORESHAJI WA DAFTARI JIMBO LA KALENGA NA ISMANI December 06, 2024
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) January 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI January 24, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MANENO MAZITO YA MHE. MHAPA WAKATI WA KUVUNJA BARAZA

    June 19, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KWA ROBO YA NNE

    June 19, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI KWA ROBO YA NNE 2024/2025 WAFANYIKA

    June 18, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI

    June 17, 2025
  • Tazama zote

Video

Makala kuhusu miundombinu ya elimu
video

Viungo vya haraka

  • FOMU YA USAJILI WA VIKUNDI
  • INGIA KWENYE MFUMO WA VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA
  • Salary slip

Viungo vinavyohusiana

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais-Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora
  • Sekretariati ya ajira
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti kuu ya takwimu huria
  • Tovuti Rasmi ya Rais

Idadi ya watembeleaji duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

https://bachelorthesiswritingservice.com

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kijiji cha Ihemi

    Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa

    Simu ya mezani: 026-2702828/2702585

    Simu ya mkononi: 0757 364 994

    Barua pepe: ded@iringadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa