Halmashauri ya Wilaya ya Iringa sasa kutumia Bajeti ya Bilioni 65.5,DC- ahimiza kilimo cha mazao ya kimkakati
Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa – DC)
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imeongezewa wigo wa bajeti yake (Celling) kutoka Bilioni 50,075,358,746 hadi 65,503,221,513 ambapo jumla ya ongezeko ni Bilioni 15,427,862,767.
Akisoma taarifa hiyo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Mkurugenzi Mtendaji Bw. Bashir Muhoja alisema “ Kwa pindi cha mwaka wa fedha 2021-2022 Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ilikisia kukusanya na kutumia jumla ya Shilingi 50,075,358,746 kutokana na vyanzo vyake mbalimbali na bajeti hii kuidhinishwa na Bunge,lakini imeweza kuongezeka kwa kiasi cha 15,427,862,767”.
Katika Mkutano huo wa Baraza wenyeviti wa kamati waliwasilisha taarifa zao na kujadiliwa na wajumbe huku taarifa ya Kamati ya Afya,Elimu na Maji ikipita bila kuhojiwa hali iliyopelekewa wajumbe wa kamati hiyo kupewa sifa kwa kazi nzuri waliofanya na kutakiwa kuongeza ubunifu na weledi.
Aidha,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mh.Stephen Mhapa alitoa msisitizo kwa Waheshimiwa Madiwani kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya mita za maji ili kuweza kutunza na kuhifadhi huduma hiyo.
“Ndugu Waheshimiwa Madiwani wenzangu hapa tuwekane sawa,haiwezakani ninyi munge mkono suala la wananchi kutokutumia mita,badala ninyi mkawe mabalozi wa kuelimisha wanannchi umuhimu wa matumizi ya mita na za maji na huu ndio muarobaini wa kuonmdoa kero na malalamiko ya kulipia maji kuliko matumizi”alisema na kuongeza;
“Kuna baadhi ya wananchi wanatumia maji ya majumbani kunyweshea mifugo au kuchimba mabwawa ya kufugia samaki wengine kutumia kama bwawa au mto katika mashamba lakini pamoja na kuwa na matumizi makubwa bado wanalalamika na kukataa kutumia mita,hii sio sawa mimi Mwenyekiti wa Halmashauri naugana na mtaalam wangu wa maji (RUWASA)kusimamia matumizi bora na sahihi ya huduma hii”alisema.
Pia,kwa nyakati tofauti wakichangia hoja Diwani wa Kata ya Maboga Venslaus Myinga alishauri kitengo cha Ukaguzi kiwezeshwe ili kiweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi hali ambayo itaondoa shaka na hata kufanya Halmashauri yetu iondoke katika uwezekano wa kupata hati yenye mashaka.
“Leo katika kablasha hatuoni taarifa ya kitengo cha Ukaguzi ukiuliza utasikia sababu ambazo zinaweza kupatiwa uvumbuzi”Alisema Mh.Myinga.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa alipana na fasi ya kutoa neon na alikuwa na haya “Wilaya yetu ya Iringa ni Wilaya ya Kimkakati hasa kwa kuwa sisi wana Iringa ni wachapa kazi,tumeamua kujielekeza katika Kilimo hususani mazao ya Parachichi, Alizeti,Soya na Mikorosho katika maeneo ambayo zao hilo lina mea hasa Isimani na Pawaga”alisema na kuongeza;
“Sote ni mashahidi kwa kipindi cha takribani miezi mitatu nyuma nchi yetu ilikubwa na uhaba wa mafuta ya kupikia na kupelekea ongezeko kubwa katika bidhaa hii naamini sisi wana Iringa Alizeti tunaweza kulima na kusaidia kushika kwa bei katika bidhaa hii na kila mwanannchi aweze kumudu gharama zake”alisema.
Aidha,Mh.Moyo aliwataka Waheshimiwa Madiwani na Maafisa Tarafa wawe mabalozi kwa wananchi wanao waongoza na kutoa elimu ya tahadhali juu ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 wimbi la tatu ambalo lipo na wananchi wasipuuze na kudharau maelekezo ya Wataalam wa masuala ya Afya.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa