Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Afunga maonesho ya Utalii Karibu Kusini
“Natoa wito kwa viongozi kuendelea kutangaza fursa za maonesho katika Mikoa yote ya Kusini kwa kuibua fursa za mazao ya Utalii na kufanya maandalizi ya kuweza kuvutia waoneshaji na wanunuzi wengi”
Kauli hii imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe alipokuwa anafunga maonesho ya Utalii Karibu Kusini Septemba 28, 2023 eneo la Kihesa-Kilolo Manispaa ya Iringa.
Mheshimiwa Kigahe ameongeza kusema kuwa, pamoja na vivutio vikubwa vilivyopo Nyanda za Juu Kusini, havitumiki sana wala kusikika hivyo kuna kazi ya ziada kuvitangaza. Utangazaji wa vivutio hivyo ndiyo nguzo kubwa ya kukuza utalii ikiwa ni pamoja na kukuza miradi mbalimbali ikianza na mradi wa Regrow.
Mh. Kigahe amesema, pamoja na jitihada za Kitaifa, kila Mkoa ujitahidi kutangaza vivutio vyake ili kukuza utalii huu, kwani kama Serikali inajitahidi kuhakikisha juhudi hizi zinafanikiwa.
Aidha, Mheshimiwa Kigahe amefurahishwa na Kaulimbiu ya Maonesho hayo inayosema “Utalii Karibu Kusini Muelekeo Mpya wa Uwekezaji” hivyo anawakaribisha wawekezaji wote waje kuwekeza katika Nyanda za Juu Kusini, kwa kujenga hotel kubwa za kisasa za Nyota Tano, na kuvutia wageni wengi zaidi wa hadhi mbalimbali kuja kutembelea Kusini.
Pia Mheshimiwa Kigahe amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa ubunifu wa kuwa na mnada wa nyama choma, kwani itasaidia wananchi kuwa na kipato zaidi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Omary Dendego ametoa shukrani nyingi kwa Waziri wa Maliasili na Utalii alipofungua maonesho hayo Septemba 23, 2023, na Wadau mbalimbali kufanikisha maonesho hayo.
Pamoja na mambo mengine Mgeni Rasmi aliweza kukabidhi tuzo kwa walishiriki katika makundi.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mbunge wa Iringa Mjini Mheshimiwa Jesca Msambatavangu.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa