Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy amefanya ziara ya kukagua kazi ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Malengamakali katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Februari 13, 2024 na kukutana na changamoto ya mfumo wa malipo changamoto ambayo imesababisha kazi kutokamilika kwa wakati.
Akitoa taarifa ya kazi Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Eng. Nico Kasililika amesema, kazi ya ujenzi ipo katika hatua ya umaliziaji ambapo suala la mfumo ndilo ambalo limekuwa kikwazo kwani fedha hazitoki kwa wakati hivyo kusababisha mafundi kutokuendelea na kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy amesema ameipokea changamoto hiyo ili kwenda kuona namna ya kufanya kazi zisikwame na wananchi wapate huduma kwa wakati.
Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Malengamakali unahusisha majengo sita ambayo ni OPD, Maabara, Vyoo, Jengo la Wazazi, Jengo la Upasuaji na Jengo la kufulia. Majengo yote haya yamejengwa kwa awamu mbili tofauti na yapo katika hatua ya umaliziaji ambapo hata hivyo jengo la OPD limeshaanza kutumika.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa