MHE. KHERI JAMES AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA LISHE 2023/2024 IRINGA DC
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James ameongoza kikao cha Kamati ya Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Agosti 26, 2024 kilichofanyika ukumbi wa makao makuu ya Halmashauri – Ihemi.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mhe. Kheri amesisitiza juu ya utoaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi katika shule zote ili kukabiliana na suala la udumavu na kwamba hakuna sababu ya kutosimamia hilo kwani Iringa inasifika kwa uzalishaji.
“Maafisa watendaji wote, maafisa lishe na wote tuliopewa dhamana katika usimamizi wa masuala ya lishe tuhakikishe tunatimiza wajibu wetu. Lishe ni wajibu wetu wa msingi sio kwa sababu kiongozi kasema wala sio kwa sababu tumesaini mikataba ya lishe bali ni sera na kwa sababu jamii isiyokuwa na lishe ina changamoto ya afya ya akili na mwili” amesema.
Aidha, Mhe. Kheri amesisitiza juu ya utengaji wa fedha kwa ajili ya masuala ya lishe na ziweze kufanya jukumu husika na kila idara kuhakikisha inafanya wajibu wake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Steven Mhapa amesisitiza kuwa ni muhimu sana wahusika wote kuyachukua maelekeza ya Mkuu wa Wilaya na kuyaweka katika utendaji ili kila mtu atoshe kwenye nafasi yake kwa kutimiza wajibu huu wa msingi.
Naye Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi Evelina Selemani amebainisha changamoto chache kuhusiana na suala la lishe ambazo ni za kufanyia kazi ili kuwa na matokeo mazuri ya tathmini ya lishe ikiwemo ushiriki hafifu wa jamii kwenye masuala ya lishe na matumizi yasiyo sahihi ya “Lengo Y”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa