Mbunge wa Jimbo la Isimani Mhe. William Lukuvi ameitisha Mkutano na wananchi wa Jimbo la Ismani Kata ya Itunundu na Kata ya Mbolimboli kwa lengo la kumshukuru Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa Kuzipatia Kata hizo Tshs. Bilioni 55 kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Mkombozi (Mifereji ya umwagiliaji) katika Kata hizo zinazopatikana Jimbo la Ismani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Ujenzi wa Mradi wa Mkombozi unatekelezwa na wakandarasi wawili (2) katika Loti nne (4).
Mkombozi Lot. 1 Mkandarasi aliekabidhiwa Mradi huu ni M/s Comfix and Engineering Ltd kwa kiasi cha fedha Tshs. 8,124,094,326.00 na kazi zinazotekelezwa ni Ujenzi wa Banio, Mfereji Mkuu (Itunundu) umbali wa kilomita 5.9 na Barabara 5.9 km
Mkombozi Lot. 2 Mkandarasi aliekabidhiwa Mradi huu ni M/s Comfix and Engineering Ltd kiasi cha Tshs. 13,462,984,502.00 kazi zinazotekelezwa ni Mfereji Mkuu (Mboliboli) - km 18, Tuta la kuzuia mafuriko- 18km na Barabara-18km.
Mkombozi Lot. 3 Mkandarasi ni M/s CRJE (EAST AFRICA) Ltd kiasi chs Tsh 15,909,720,607.94 kazi zinazotekelezwa ni Mfereji wa kati (Secondary Canal) kilomita 39.99 na Mifereji ya Mashambani (Tertiary Canal) kilomita 90.219
Mkombozi Lot. 4 Mkandarasi ni M/s CRJE (East Africa) Ltd kiasi cha Tshs. 17,991,711,315.00 kazi zitakazotekelezwa ni Mfereji ea kati (Secondary Canal) kilomita 20.79 na Mifereji ya Mashambani (tertiary canal) kilomita 78.2.
Utekelezaji wa ujenzi huu kwa loti zote ni wa muda wa miezi kumi na nane (18) kuanzia tarehe 01/09/2022 na kutegemewa kukamilika tarehe 29/02/2024.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa