Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mhe. Paulo Makonda amewataka viongozi mbalimbali kwenye Mikoa, Wilaya na Halmashauri kueleza vitu halisi vilivyofanyika kwenye eneo husika kama matokeo ya fedha nyingi zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mhe. Makonda ameyasema hayo alipokuwa kwenye ziara mkoani Iringa Februari 08, 2024 katika viwanja vya Mwembetogwa kama mwendelezo wa ziara zake za kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
“Mwoneshe mwananchi matokeo ya kazi iliyofanywa na hizo fedha aweze kuona ni mali yake, kutaja idadi ya fedha tu haisaidii yaani kutaja tu kuna mabilioni yameletwa kwa mwananchi wa kawaida hizo lugha hazielewi bali anachohitaji kusikia ni manufaa ya uwepo wa CT Scan, vituo vya afya, Hospitali, uwanja wa ndege, pembejeo na vifaa vya kilimo na namna vinavyoweza kuwanufaisha”
Eidha, Mhe. Makonda amewataka watendaji wa serikali wa kuchaguliwa, kuajiriwa au kuteuliwa kueleza kazi wanazozifanya na faida zake kwa wananchi na kutumia vyombo vya habari ili kuwahabarisha wananchi kazi zinazofanyika.
“Sisi Kwenye chama tungefurahi kuwaona watendaji wa serikali hii ya Dkt. Samia kwa kuwa ninyi wenyewe ni mashuhuda ya kwamba mambo mazuri yanafanywa katika maeneo yenu, kwenye idara zenu na pesa zinaletwa kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya wananchi, msisuburi mpaka aseme Waziri peke yake kila mtu ana wajibu wa kuisemea idara yake”.
Mhe. Paulo makonda pia amepata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi hususani kwenye masuala ya migogoro ya ardhi na kuzitafutia ufumbuzi.
Sanjari na hayo, Mhe. Makonda amewaasa viongozi wa serikali kutengezeza mazingira ya kuyatangaza maeneo yao ya kiutalii na kuwafanya wananchi nao wajisikie fahari kwao kuwa Watanzania na kwa hiyari yao nao watangaze vivutio vilivyopo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa