Mwenyekiti Mhapa Awataka Watumishi Kutulia Kwenye Vikao
Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa Robo ya Kwanza kwa mwaka wa Fedha 2024/2024 umefanyika Novemba 08-09, 2024 kama kanuni zinavyotaka kufanya Mkutano wa Baraza kila baada ya miezi mitatu.
Awali mkutano wa Baraza ulitangulia kwa kutoa taarifa za Kata kwa Kila Diwani na kuziwasilisha katika Mkutano ambao ulifanyika Novemba 08, 2024 na siku ya pili ya Novemba 09, 2024 kufanyika kwa Baraza kamili la Madiwani.
Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Stephen Mhapa amewataka Watumishi kutulia kwenye vikao na siyo kutoka nje kila mara kwa visingizio mbalimbali, hali inayopelekea kukosa kupokea maagizo kwa wakati na kushindwa kujibu maswali ambayo yanaulizwa katika Mkutano huo, kutokana na kukosa utulivu katika mkutano.
Kutokana na hilo Mhe. Mhapa amemtaka Mkurugenzi kuwachukulia hatua wale ambao wanakiuka kanuni za kutosikiliza mkutano na kushindwa kutoa majibu katika mkutano.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James amewataka Madiwani hao kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za uchaguzi zinazoendelea hivi sasa kwani ni ajenda kuu kwa kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajia kufanyika Novemba 27, 2024
Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Robert Masunya amekiri mapungufu yaliyotokea katika mkutano huo na kupokea maagizo yote yaliyotolewa katika Baraza hilo na kuahidi atayafanyia kazi
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa