Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mei 19, 2025.
Maeneo ya miradi yaliyotembelewa ni mradi wa kiwanda uzalishaji wa vyakula vya wanyama cha Shafa Mills, ukarabati wa mradi maji kijiji cha Malizanga, ujenzi wa barabara ya Iringa - Msembe yenye urefu wa km 104 inayojengwa kwa kiwango cha lami, ujenzi wa mabweni mawili shule ya sekondari Makifu, na ujenzi kituo cha Mahuninga.
Katika ziara hii Mkuu wa Mkoa Mhe. Peter Serukamba amesisitiza wasimamizi kuweka mkazo kwenye suala la ubora ili miradi hiyo iweze kudumu pale inapokuwa imekamilika.
Aidha Mhe. Serukamba ametoa pongezi na shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na serikali kwa miradi inayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Iringa - Msembe ambayo imekuwa kwenye mpango kwa muda mrefu.
https://www.instagram.com/p/DJ3TXw-M4pY/?igsh=MWIzd3RtdzZzMG5o
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa