Waziri wa Maliasili na Utalii Azindua Rasmi maonesho ya Utalii Karibu Kusini Mkaoni Iringa
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Angella Kairuki amezindua rasmi Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Kihesa-Kilolo Manispaa ya Iringa Sepemba 23, 2023.
Akizungumza katika uzinduzi huo ameeleza kwamba, ni jukumu la kila mmoja kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Dkt, Samia Suluhu Hassan ili kuendelea kulinda Sekta ya maliasili na kufikia lengo kw mikakati iiliyokusudiwa.
“Sekta ya Utalii ni chanzo kikubwa cha ongezeko la mapato nchini Tanzania, hivyo kuendeleza na kulinda ni moja ya lengo la kutimiza mikakati ya Utalii Karibu Kusini” amesema Mh. Kairuki.
Aidha, ameongeza kusema kuwa, miundombinu ya barabara itaboreshwa ili kuendelea na kukuza Utalii Kusini.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Omary Dendego, ametoa rai kwa wananchi kushiri kikamilifu katika maonesho ili kuweza kutangaza fursa na kujifunza mambo mbalimbali.
Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yana Kaulimbiu isemayo, “Utalii Karibu Kusini, Mwelekeo Mpya wa Uwekezaji”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa