Mheahimiwa Mhapa Asisitiza Usimamizi wa Miradi
Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe Steven Mhapa ameongoza mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani kwa Robo ya Tatu kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mkutano huo umefanyika leo Mei 27, 2024 ambapo utaendelea hadi kesho Mei 28, 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri wa Siasa ni Kilimo, ambapo leo siku ya kwanza ni kuwasilisha taarifa za Kata.
Pia Mhe. Mhapa amesisitiza kuwa Wakuu wa Idara wawe tayari kupokea Taarifa ya miradi ya maendeleo na kuhakikisha kuwa Miradi hio haitakiwi kuvuka mwaka na kuhakikisha kuwa wanapata Taarifa Kila siku juu ya maendeleo ya mradi.
Vilevile Mhe. Mhapa amewataka Madiwani kuhakikisha kuwa wanasimamia miradi hio kwa imakini mkubwa kwa kuwa miradi wako nayo karibu huku wakisaidiana kupeana taarifa na Wataalam ili kufanikisha miradi hiyo
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa