Milioni 247,900,000/= Kutolewa katika Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imetenga kiasi cha Tsh. 247,900,000/= kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu ikiwa ni kutekeleza agizo la utengaji wa asilimia kumi (10%) ya fedha za mapato.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bibi Saumu Kweka amewapongeza wote walioshinda katika mchakato wa maombi ya mkopo, amesema lengo lilikuwa kubwa lakini hata kwa hicho walichokipata yawapasa kushukuru.
Aidha amesema kuwa mikopo hiyo watakayipatiwa itakaa kwa muda wa miezi mitatu ndipo marejesho yataanza.
"Ninawaomba hizi fedha mlizoomba mkafanyie kazi mliyoombea ili muweze kurejesha kwa wakati na ili wengine waweze kukopa na wao wafanye maendeleo".
Pia amesema mikopo yote itakayotolewa haitarejeshwa kwenye akaunti kama zamani kwani kwa sasa kutakuwepo na namba maalumu kwa ajili ya marejesho.
"Kwa sasa tuna utaratibu mpya hivyo hakikisheni mtu mnayemtuma akaweke fedha kwenye akaunti ni lazima alete risiti ili kujua kweli kiasi kilichowekwa ndicho kile mlichokubaliana".
Kadhalika Bibi Kweka amewataka wanufaika wa mikopo kuwa makini katika mafunzo yatakayotolewa yakiwemo unyanyasaji na ukatili wa kijinsia, namna ya kufanya buashara, na masuala mengine ya kijamii kwani yana manufaa makubwa katika maisha ya kila siku.
Vikundi takribani 56 vitanufaika na mikopo hiyo ikiwa vikundi vya wanawake ni 18, vikundi vya vijana ni 19 na vikundi vya watu wenye ulemavu ni 19 ambapo jumla ya vikundi vyote vitahamishiwa fedha katika akaunti za vikundi husika.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa