Mkaa na Kuni Sasa Baaasiiii!
Mjadala wa siku mbili wa tarehe 01 – 02 Novemba, 2022 umeandaliwa kujadili matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika jamii yetu.
Mjadala huo ambao umeandaliwa na Wizara ya Nishati ukiongozwa na Waziri mwenye dhamana Mheshimiwa Januari Makamba, na kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, umesisimua wajumbe na washiriki kwa kutoa mawazo chanya juu ya nini kifanyike katika kuendeleza nishati hii ya gasi.
Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi Mheshimiwa Rais amesema” mjadala huu ni wa kihistoria na umkuja wakati muafaka katika kipindi hiki cha kizazi cha sasa. Mkutano huu ulipangwa kuhudhuriwa watu 1000 lakini kutokana na umuhimu wake watu zaidi ya 3000 wameweza kujiandikisha, hii inaonesha kuwa watu wana juu ya jambo hili”
Mheshiwa Rais ameendelea kusema kuwa, “nawapongeza Mikoa yote iliyoshiriki katika mkutano huu kwa njia ya mtandao ambayo ni Dar es salaam,Shinyanga, Iringa na Tabora. Nawakaribisha kutoa mawazo yenu ili kuleta mtazamo chanya katika matumizi ya gesi nyumbani”
Mheshimiwa Samia ameendelea kusema, “kwa nini nishati safi? Kwa sababu njia hizi zinazotumika sasa za kupikia mkaa na kuni huleta changamoto kiafya, na Wataalamu wametueleza athari za kutumia njia hizi.” Mh. Samia amesema.
Pia tatizo la mazingira, mgao wa umeme na maji hii yote husababisha na ukataji miti na kuchoma mkaa na kusema kuwa, Mkoa wa Pwani unaoongoza kwa kukata miti na kusababisha matatizo na kukauka kwa mito hasa mto Ruvu.
“Tunapokata miti tunasababisha gharama kubwa za maisha zaidi, mfano kwa mwanamke kienda kutafuta kuni anaweza akabakwa huko porini, unapigwa kwa sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani, kukutana na wanyama wa pori na kuweza kuwadhuru, na mambo mengine yanayohatarisha maisha yao na matumizi ya kuni huhatarisha afya”.
Kubwa moja ni kubadilisha mtazamo ambapo kwa mfano nyumba uzuri lakini lazima ujenge jiko la nje, ili tu uweze kutumia jiko la kuni. Sasa hivi si jambo la kufumbia macho ni lazima tutekeleze afua hizi za nishati. Takwimu zinaonesha wananchi wanaotumia nishati ya gasi ni 5% umeme 2%.
Mheshimiwa Rais ameelekeza kuwa, utatuzi wa Kisera umechukulia suala hili si la muda mfupi, lazima tuanze sasa tena kwa kasi kubwa. Kianzishwe kikundi kazi ambacho kitashughulikia nishati safi, na si kwa Serikali peke yake, pamoja na Sekta Binafsi, Maendeleo ya Jamii na TAMISEMI kusikilize Sekta Binafsi wanasemaje kwani ndiyo fursa yao katika jambo hili.
Kikosi kazi hiki kitakuja na suala moja la suluhu ya mpango wa matumizi ya nishati safi na endelevu. Kikosi kazi hiki kitaratibiwa na Wizara ya Nishati.
Mheshimiwa Rais pia amesema ni lazima twende na nishati safi ya kupikia kukinga wanawake ambao wanapata madhara makubwa na hawalipwi chochote, sasa angalau tuwapunguzie madhara wanayopata. Pia itasaidia kupata muda wa kufanya shughuli la kiuchumi. Kikosi kazi hiki kitakuwa cha Kitaifa ambacho kitaratibiwa Kitaifa zaidi. Tanzania tumejiingiza kwenye mambo kadhaa kwa mpango wa Women Rights in Justice hii itampa mwanamke muda wake, kwamba sisi ni Machampion. Mkakati huu utadumu miaka 10 ili 80-90% wawe katika nishati safi ya kupikia, kinachotakiwa ni kutoa elimu kwa wananchi ili waelewe madhara ya kutumia kuni na mkaa.
Sisi Serikali tutafanya bajeti ambayo itaanzisha Mfuko wa Nishati Safi ya Kupikia kama ilivyo kwenye Kampeni ya Kumtua Mama Ndoo ambayo imefikia 80%. Mpango huu utatoa mchango wa Mashirika ya Wadau wa Maendeleo.
Mikoa inayoongoza kwa kukata miti ya asili ni Pwani, Morogoro, Tabora, Lindi na Ruvuma kwa kisingizio ni bei rahisi ya mkaa. Miti mingi tunayotakiwa kupanda ni miti ya matunda. Hii itasaidia kuzalisha asali ambayo ni hitaji la Dunia.
Nilielekeza kuwa Taasisi zinazotumia zaidi ya watu 300, ni lazima watumie Gesi ili kuzuia kutumia nishati chafu. Ifikapo 2024, nataka nisimame kwa wananchi kuwa nimefanya mambo mbalimbali ikiwemo jambo hili la nishati safi ya kupikia.
Mheshimiwa Rais amemaliza kwa kusema, “Tunahitaji nishati safi na salama ya kupikia kwani italeta ufanisi wa Afya Bora kwa Jamii Yetu”.
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluh Hassani kufungua mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ameongoza mjadala huo kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya waliopo Mkoani humo.
Katika mjadala huo Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Makamu Wenyeviti na wadau mbalimbali, wameweza kutoa ushauri juu ya nini kifanyike ili kuweza kuepukana na ukataji wa misitu na ni namna gani kama Watanzania tunaweza kuongeza matumizi ya gesi ya nyumbani.
Moja ya ushauri waliotoa Wadau kwa Serikali ni kuweza kuweka ruzuku kwenye gesi na vifaa vyake jambo ambalo litapelekea gesi kuuzwa kwa bei ya chini ambapo wananchi wengi wataweza kununua na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa