Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndugu Robert Masunya amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wakili Bashir Muhoja ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea. Makabidhiano hayo yamefanika katika Ukumbi wa Halmashauri – Ihemi yakishuhudiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Steven Mhapa Machi 21, 2024.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri mara baada ya zoezi la makabidhiano Ndugu Robert Masunya amesisitiza juu ya masuala muhimu ya kupewa kipaombele ambayo ni ukusanyaji wa mapato, lishe, ukatili wa kijinsia na hoja za uaguzi, mambo ambayo ni ya kusimamiwa kwa ukaribu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Steven Mhapa ametoa neno la ukaribisho kwa ndugu Robart Masunya ambaye amekabidhiwa ofisi na kutoa neno la shukrani kwa Wakili Bashir Muhoja kwa utumishi wake akiwa Iringa DC na kumtakia kheri anapoenda kwenye kituo chake kipya. Mhe Mhapa pia amewaasa watumishi kuishi vizuri na watu wote kwani hawawezi kujua yatakayojiri kesho.
Naye wakili Bashir Muhoja amewashukuru watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na Baraza la Madiwani kwa ushirikiano waliouonesha kwa muda wote wa kutekeleza majukumu ya kazi na kuweka wazi kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano ikiwa kuna jambo la kiutendaji linalohitaji ufafanuzi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa