MAKAMPUNI YA ASAS YAUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA COVID 19 IRINGA DC
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano Iringa DC)
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imepokea msaada wenye thamani ya Shilingi milioni 14 kutoka makampuni ya ASAS kwa lengo la kuimarisha utowaji wa huduma za afya hasa kwa Ugonjwa huu wa COVID 19.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw Robert Masunya amesema Halmashauri imepokea maelekezo kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutenga kituo maalum kwa ajili ya kutolea huduma kwa wagonjwa wa Corona.
“Hadi sasa Halmashauri haina mgonjwa ila tumepokea maelekezo na tunafanya maandalizi iwapo itatokea basi hakutakuwa na wasiwasi ya wapi tutawaweka wagonjwa na kuwahudumia kwa kuwa eneo hili la Zahanati ya Kising’a ndio litatumika”alisema.
Bw Masenya alisema ukarabati wa kituo hiko utahusisha kujenga uzio wa wodi maalum ambayo inajumla ya vitanda kumi na sita (16) ambavyo vitanda nane kwa ajili ya wagonjwa wakiume na vingine nane kwa wagonjwa wa kike,na kuongeza ujenzi wa vyumba maalum vya kubadilishia nguo baada ya kuwahudumia wagonjwa na vyumba vya kujisafishia .
“Kutakuwa na milango miwili wodi mlango mmoja wa kuingilia na mwingine kutokea ili kuzuia usambaaji wa virusi vya CORONA,lakini pia kwa kuweka uzio tutadhibiti wagonjwa waliopta nafuu kutoroka na kurudi katika jamii zao bila kuruhusiwa na wataalam wa afya”alisema.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Samwel Marwa alisema mbali na Wodi yenye vitanda 16 kuna chumba maalum chenye vitanda vine ambacho kitatumiwa kwa washukiwa wa virusi vya Corona wakati wa kusubiri majibu ya sampuli kutoka maabara kuu ya Taifa.Akijibu swali la Mwanahabari Bw Marwa alisema “washukiwa wa virusi vya COVID 19 walikuwepo lakini kama livyozungumza Mkurugenzi Bw Masunya majibu ya sampuli yalionyesha hawana maambuziki hivyo waliruhusiwa kurudi katika jamii zao baada ya muda wa matazamio kuisha bila kuonyesha dalili za ugonjwa huo.”.
Bw Masunya pamoja na Kuyashukuru Makampuni ya ASAS amewaomba wadau wengine wajitokeza kuchangi ili kuisaidia Serikali kupambana na Janga la virusi vya COVID 19 ambavyo ni hatari zaidi kwa afya ya Binadamu.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa