MKURUGENZI MTENDAJI ATETA NA WATENDAJI WA KATA IRINGA DC
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndg Robert Masunya amefanya kikao na watendaji wa kata katika Halmashauri na kuwakumbusha kuwajibika vema kwenye nafasi zao kama wakurugenzi wa maeneo yao na hivyo watendaji wa kata wanawajibika kwa watumishi wengine wa chini yao.
Aidha Ndg. Masunya amewahimiza watendaji wa kata kuwa wana wajibu mkubwa wa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuzuia matumizi ya fedha mbichi kwenye kata na vijiji kwani kutumia fedha mbichi isiyopita kwenye mfumo ni kosa kisheria na linaweza kumgharimu mtumishi.
“Tuanze ukurasa mpya wa uwajibikaji, kwenye nafasi uliyopewa usipofanya vizuri inaweza kuondoka na sio marupurupu unayopewa usipoyachukua unaweza kuondoka”
Naye Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Bi. Caroline Ang'wen Otieno amesema, Jukumu letu ni kulea watumishi, na tupo tayari kumuunga mkono Mkurugenzi kazi ifanyike nasi tutoe ushirikiano tuanze ukurasa mpya na ikiwa kuna changamoto tushirikishane. Lengo tusimame pamoja kuongea lugha moja na sio kuviziana vivyo kwa kwa watumishi wengine ngazi ya kata na vijiji.
Kikao cha Watendaji wa kata na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kimekuwa na lengo la kupitia tathmini ya hali ya utendaji hasa suala la mapato, kukumbushana mambo muhimu ya kiutendaji, wajibu wa kila mtumishi na kuchukua hatua ya pamoja.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa