Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Mhoja amefanya ziara na kuzungumza na Watumishi watumishi wa Kata ya Kalenga, Ulanda, Nzihi na Kiwele katika Tarafa ya Kalenga. Mkutano huu umefanyikia katika ukumbi wa chuo cha Nursing Tosamaganga 13.12.2023 ambapo lengo la ziara ni kuwakumbusha watumishi wajibu wao, haki zao na kusikiliza changamoto ili kuzipatia ufumbuzi.
Mkurugenzi Mtendaji pia aliambatana na wataalamu idara na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kila jambo linalomgusa mtumishi linasikilizwa na kupatiwa ufumbuzi, wataalamu hao ni pamoja na Mtaalamu wa Saikolojia, Mtaalamu kutoka NHIF, PSSSF, WCF na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) ambao wameweza kufafanua masuala mbalimbali yanayowagusa watumishi.
Wataalamu kutoka idara na taasisi mbalimbali wamefanya uwasilishaji wa masuala mbalimbali yanayowahusu watumishi kisha Mkurugenzi kutoa nafasi kwa watumishi hao kuuliza maswali na kutoa changamoto zao ili kupatiwa majibu au ufumbuzi
Akisungumza na watumishi, Mkurugenzi Mtendaji (W) Wakili Bashir Mhoja amesema “Tumesikiliza na kupata hata nafasi ya kusoma kila kilichoandikwa kwenye kila karatasi, Lakini na yale maswali yaliyoulizwa moja kwa moja pia tumepata nafasi ya kuyajibu pia kuna ambayo tumeyabeba tunaahidi kuwa tutarejesha mrejesho kwa maandishi aidha kwa viongozi wa Hospitali au wa taasisi husika kwa maana ya shule zetu au mtu mmoja mmoja”
Ziara hii inaendelea kwenye Tarafa ya Isimani ambapo Mkurugenzi Mtendaji (w) na timu yake ambapo atakutana na watumishi kutoka Kata ya Malengamakali, kihorogota na Kising’a na Nyangoro.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa