Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndugu Robert Masunya afungua mafunzo ya watumishi wa ajira mpya yaliyofanyika katika ukumbi wa makao makuu Ihemi Agosti 28, 2024.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ndugu Robert Masunya amewakumbusha watumishi wa ajira mpya kuwa wanapaswa kutambua kuwa wameletwa kufanya kazi kwa lengo la kuisaidia Serikali na sio tu wao kujiona wamepata ajira.
“Serikali imewaleteni ili muisaidie kufanya kazi sio imewasaidia ajira na ninyi muwe sehemu ya waajiriwa, kwa hiyo serikali imewaleta muifanyie kazi ili tija itokee na hapo hapo kwenye kuisaidia serikali ndio suala la ajira linatokea” amesema.
Aidha ndugu masunya amewaasa watumishi hao kujikita kwenye miongozo na taratibu za kitanzania na kiutumishi waumma badala ya kuleta tabia binafsi ambazo hazipo kwenye taratibu na sharia za nchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imepokea watumishi wapya 15 kwa awamu ya kwanza ambao wamepatiwa mafunzo sanjari na watumishi wengine walioajiriwa kuanzia 2022 hadi 2024 ili kuwaongezea uelewa wa mazingira na uwajibikaji katika majukumu yao mbalimbali.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa