Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndugu Robert Masunya ameongea na vijana ambao ni wafanyakazi wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhusu mambo mbalimbali yanayowahusu vijana Agosti 14, 2024
Ndugu Masunya amesema vijana wana changamoto nyingi sana hasa katika masuala ya mahusiano lakini pia wana fursa za kuweza kuwa bora wawapo kazini hivyo lazima wawe makini kwa mazingira yanayowazunguka na mahusiano wanayoyaanzisha.
“Future ya ujana wenu ni uzee na future ya ujana wenu inategemewa na namna gani unayaandaa maisha yako sasa kuelekea kule kwenye uzee wako. Wakati wa ujana ni wakati ambao kijana anayatengeneza maisha yake ya baadaye hivyo inahitajika uangalifu kwa wewe mwenyewe na kwa jamii inayokuzunguka” amesema.
Aidha amesema ili kijana awe na ubora na wa thamani inategemea na namna anavyoishi, anavyoenenda na namna anavyofanya kazi na kutoa matokeo.
Vilevile Ndugu Masunya amesema kwamba lengo la kikao hiki ni kuwakumbusha vijana wajue kuwa wao ni nguvukazi ya Taifa, nguvukazi ya familia na wategemezi wao na kwamba vijana ndio wanaotegemewa na Taifa, familia, na hata wategemezi wengine hivyo kila mmoja anapaswa kutengeneza thamani yake yeye mwenyewe kwa kufanya kazi kwa bidi na kujitunza.
Kwa upande wao, vijana walioshiriki wamepongeza na kushukuru juu ya wito wa kikao hiki na kusema kuwa ni kizuri, kinawajenga na ikiwezekana ipatikane siku nyingine ili kuwa na kikao kama hicho kitakachotoa fursa ya kuzungumza Zaidi na kutoa changamoto zao kama vijana.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa