Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja amepata wasaa wa kuongea na watumishi wa kada mbalimbali katika Tarafa ya Isimani kwa Kata za Malengamakali, Kihorogota, Kising’a na Nyang’oro mapema 14.12.2023. Wakili Muhoja ameambatana na wataalamu wa Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali ili kushughulikia kila changamoto ya mtumishi.
Taasisi zilizokuwepo ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Jeshi la Polisi, na Mtaalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Iringa ambao waliwasilisha maada zao na baadaye kujibu maswali na hoja za watumishi.
Akizungunza mara baada ya kupokea hoja na changamoto za watumishi, Wakili Muhoja amewahakikishia watumishi kuwa hoja na changamoto zote zilizochukuliwa zitaenda kufanyiwa kazi na mrejesho utatolewa kwa kila aliyewasilisha changamoto yake kwa maandishi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Bi. Beatrice Augustino amefafanua kuhusu Kanuni Mpya za Utumishi wa Umma za Mwaka 2022 ambazo tayari zimeshatangazwa kwenye gazeti la Serikali na kwamba hizo ndizo kanuni ambazo zitakuwa zinatumika kama rejea badala ya zile za mwaka 2003.
Ziara hii ni mwendelezo wa ziara za Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambazo zinalenga kuwafikia watumishi, kuwasikiliza na kutatua kero na changamoto balimbali zinazowasibu katika utumishi wa Umma sanjari na kufafanua masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa