Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndugu Robert Masunya ameongoza kikao cha wadau wa Asasi zisizo za kiserikali zinazofanya kazi katika eneo la Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Mei 28, 2024.
Katika kikao hicho, kila Asasi imesoma taarifa za utekelezaji wa shughuli zake sanjari na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Ndugu Masunya amesisitiza kuwa Asasi zinapaswa kuzingatia maadili wakati wa utekelezaji wa shughuli zao na kwamba, Halmashauri inatambua michango yao na kuahidi kuwa changamoto zote zilizotolewa na baadhi ya Asasi zimepokelewa na zinaenda kufanyiwa kazi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa