TASAF yafanya Uhakiki ili kubaini Wanufaika Hewa.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa -DC)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bi. Josephine Joseph amesema katika kipindi cha pili cha Mradi wa TASAF awamu ya tatu wanafanya uhakiki ili kubaini wanufaika hewa.
Bi.Joseph amesema hayo wakati akisoma taarifa fupi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw.Robert Masunya,Wakuu wa Idara na Vitengo ili kwa pamoja waweze kusimamia utekelezaji wake na kunusuru kaya hizo kama serikali inavyokusudia.
“Utekeezaji huo utafanyika katika Halmashauri zote I85 za Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar na itahusisha Vijiji,Mitaa na Shehia zote ambazo hazikupata fursa katika utekelezaji wa kipindi cha kwanza ambacho kimekalimilika Disemba 2019”alisema.
“kipindi cha pili kitafikia kaya milioni moja laki nne na hamsini elfu zenye jumla ya watu milioni saba kote nchini hii ikiwa ni nyongeza ya kaya laki tatu na hamsini elfu,ambapo mkazo mkubwa utakaofanywa katika kaya hizi ni kufanya kazi ili kuongeza kipato”aliongeza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Robert Masunya amesisitiza kazi ya uhakiki ifanyike kwa kuzingatia weledi wa Utumishi wa Umma na kuhesimu mipaka ya kazi iliyoainishwa kisheria.
“Ni kosa kutumia urasimu wa udugu na urafiki katika utekelezaji wa kazi na badala yake kazi hii ifanyike kwa mujibu wa sheria,taratibu na miongozo itakayotolewa na TASAF ili kuleta tija iliyokusudiwa na Serikali”alisema.
Bw.Masunya ametoa Rai hiyo Juni 29 mwaka huu,kwa wasimamizi ambao wemejengewa uwezo ili wakatoe elimu hiyo kwa wanufaika wa TASAF ili nao waweze kujikwamua na kutoa mafanikio chanya na kuacha alama ya unufaika wa mradi huo wa TASAF.
“Nawasihi sana kazi hii muifanye kwa moyo mkubwa,uadilifu na uaminifu mkubwa zaidi kwa kuwa sasa hivi ni kwenda kumalizia maeneo ambayo ni ya msingi zaidi ili kuisaidia Serikali kuwafikia walengwa stahiki”alisema Bw.Masunya.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa