Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa yaipongeza Iringa DC kwa utekelezaji wa Miradi yenye ubora.
Ummi Mohamed (Afisa habari na Uhusiano,Iringa-DC)
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tarehe 18 Januari mwaka huu ambapo ilitembelea shule zilizojengwa kwa pesa ya tozo, mradi namba 5441 TCRP na madaraja.
Akizungumza wakati wa kukagua miradi hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh.Abel Nyamahanga amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi yote na kuongeza kuwa imezingatia thamani ya fedha (Value for money).
“Nichukue fursa hii kuwapongeza viongozi wote wa Serikali kuanzia Mh.RC,DC,DED na Wataalam wote hakika mmefanya kazi nzuri tunatambua uharaka wa miradi hii lakini mmefanya vizuri sana nawapongeza sana”alisema Mh.Nyamahanga.
Kwa upande wa miradi inayotekelezwa na Halmashauri ambayo ni sehemu ya vitega uchumi ni nyumba mbili zinazojengwa eneo la Gangilonga Manispaa ya Iringa,mradi ambao ukikamilisha utachangia sehemu ya mapato ya ndani.
Aidha,Mh. Nyamahanga alikagua miradi ya maji katika Kata ya Maboga Kijiji cha Magunga,Mradi wa daraja unaounganisha Vijiji vya Bandabichi na Itengulinyi sambamba na miradi ya tozo, miradi namba 5441 TCRP.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh.Queen Sendiga ameishukuru Kamati hiyo na kuahidi kuendelea kutekeleza vyema miradi yote ambayo imeainisha katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo ipo katika eneo lake la Uongozi.
“Nimepokea maelekezo katika baadhi ya miradi nitayafanyika kazi ili kuboresha zaidi lakini pia na mimi niwapongeze sana Watumishi wangu kwa kujitoa kwenu nakiri kufahamu baadhi yenu mlifanya kazi zito usiku na mchana ili kuhakikisha miradi hii inakuwa na ubora tuliokubaliana na kutarajiwa ili thamani ya fedha za Mh.Rais Samia Suluhu Hassan ionekane”alisema na kuongeza
“Shukrani yetu kwa Mh.Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuitunza miradi hii na kuhakikisha inakuwa katika mazingira ya usafi ili iendelee kupendeza kama inavyoonekana wakati huu”alisema Mh.Queen Sendiga.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa