Baraza la Madiwani Laidhinisha Taarifa ya Hesabu za Mwaka wa Fedha Unaoishia Juni, 2023
Baraza la Madiwani leo Agosti 30, 2023 limepitia na kuidhinisha taarifa ya hesabu za mwisho za Halmashauri ya Wilaya ya Iringa za mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2023.
Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Julius Mbuta, na Katibu wake ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Saumu Kweka.
Akitoa hotuba yake fupi Mheshimiwa Mbuta amesema, “tunawaamini wataalam wamefanya kazi vizuri ya kusimamia na kulinda rasilimali za Halmashauri. Pia kuna makosa madogodogo yarekebishwe ili hesabu ziwe sawa”.
Taarifa zilizopitishwa ni zile za mizani ya hesabu, ufanisi wa hesabu na mtiririko wa fedha. Pia mabadiliko ya rasilimali za Halmashauri na za ulinganufu wa bajeti na halisi.
Akiwasilisha taarifa hiyo ya hesabu Kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bi. Jwan Maria Yengi amesema, “baada ya kuidhinisha ninyi Waheshimiwa Madiwani, hesabu hizi ziko tayari kuwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali”.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya Ndugu Semindu Michael amesema, “Madiwani mnafanya kazi vizuri ya kusimamia wananchi na miradi inayotelekezwa katika Kata zenu. Pia mmepewa jukumu la kujua kila mradi unaoingia katika Kata, na kujua kiasi cha pesa kinachotekeleza katika mradi husika. Hivyo mnaisaidia Serikali kwa kiasi kikubwa sana kwani ninyi mpo karibu na wananchi kwa kujua mahitaji yao”.
Pamoja na hayo Ndugu Semindu ametoa maagiza kwa Madiwani hao kuwa, wasimamie na kufuatilia wafanyabiashara wa mafuta kuelekea bei mpya, kwani kuna baadhi yao huwa wanaficha mafuta na kusubiri bei ipande. Kadhalika amewaagiza Maafisa Tarafa wafanye utaratibu wa kushghulikia kero za wananchi katika maeneo yao kwa kushirikiana na Wataalam.
Ndugu Semindu ametoa pongezi kwa Mkoa wa Iringa kwa kuwa mshindi wa Tatu Kitaifa katika kushughulikia Afua za Lishe, na kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imekuwa ya 48 katika suala la Lishe.
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya (CCM), Komredi Costantino Kihwele ameeleza kuwa, walipofanya ziara kukagua miradi ya maendeleo walifurahishwa sana kwa kukuta wananchi na wanachama wa CCM katika kila eneo la mradi. Hii imeonesha ni jinsi gani Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa kwa kufuatilia miradi inayoletwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Pia amepongeza kwa miradi hiyo kuwa vizuri, na kutoa dosari ndogo ambazo ni rahisi kurekebisha.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa