MKUU WA MKOA WA IRINGA AFUNGUA MAFUNZO YA SHIMIWI
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amefungua Mafunzo ya Viongozi, Walimu na Madaktari wa Michezo wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo Iringa tarehe 22.06.2023 na kuhitimishwa tarehe 23.06.2023.
Akifungua mafunzo hayo Mhe. Dendego amesema rushwa haikubaliki katika michezo kwani kwa kufanya hivyo tunaleta huzuni, chuki, hasira lakini pia ni kuua vipaji na kupitia mafunzo haya utekelezaji wa kwa vitendo utaenda kufanyika yaani aliyeshinda apewe ushindi wake na aliyeshindwa ashindwe kwa haki.
Aidha Mhe. Dendego amekaribisha mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Iringa kwa mwaka 2023 “Sisi ndugu zenu wa Iringa tupo tayari kuwapokea, huduma zetu mtazikuta tumezitayarisha kwaajili ya kuwapokea, mtakaa salama, mtacheza salama, mtakula salama, mtalala salama, na tutamwomba Mwenyezi Mungu awasafirishe salama wote waliokuja walipotoka na kurudi kakini pia tutawapa burudani za kutosha za Kihehe” amesema.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa, Bi Tika Mwakenja amesema, Mafunzo haya yanatolewa kwa watu mia moja ambao ni viongozi wa kamati ya utendaji wa SHIMIWI Taifa, Wajumbe wa Sekretariet ya SHIMIWI Taifa, Viongozi wa Kamati ya Utendaji wa Vilabu, Walimu wa mpira wa miguu na netiboli pamoja na Madaktari wa michezo wa vilabu vya michezo ya SHIMIWI
Lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo katika shughuli za michezo mahali pa kazi pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali za utekelezaji wa majukumu, kukumbushana kanunu za michezo, umuhimu wa tiba kwa wanamichezo pamoja na Mada kuhusu mapambano dhidi ya rushwa katika michezo Tanzania.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa