Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amefanya kikao na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Waheshimiwa madiwani, maafisa tarafa na viongozi wengine wa Wilaya katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo April 08, 2024.
Katika kikao hicho Mhe. Serukamba ametumiafursa hiyo kujitambulisha, kuwatambua viongozi anaofanya nao kazi na kujua shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na hatua za utekelezaji wake.
Akizungumza na viongozi hao wa Mhe. Peter Serukamba amewaomba waweze kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa kwenye maeneo mbalimbali ya wananchi inakamilishwa kwa wakati na kwa ubora unaostahili.
“Tunapata fedha nyingi kutoka Serikalini kwa hiyo tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii. Naona miradi mingi ipo nyuma hivyo tunatakiwa kuikamilisha miradi ifikapo April 30, 2024”
Pia amemtaka Mkurugenzi Mtendaji aweze kufunga hoja za CAG kwa wananchi, na kwamba kila malipo yanayofanyika kuwepo na mikataba, invoice na kufuata taratibu.
Kwa upande mwingine Mhe. Peter Selukamba ametoa maelekezo kwa viongozi na wakuu wa idara kuhakikisha kuwa wanasikiliza na kutatua kero za wananchi, kusimamia asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri yaliyolenga kwenda kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Na kutoa rai kwa waheshimiwa madiwani washirikiane na wataalamu kuhakikisha kuwa wale waliokopafedha za 10% wanafanya marejesho ili kutoa fursa kwa wengine kukopa.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Steven Mhapa amemuahidi Mkoa wa Mkoa Mhe. Peter Serukamba kuwa maelekezo yote aliyoyatoa wameyapokea na watahakikisha wanayafanyia kazi kwa niaba ya wafanyakazi na kwa Halmashauri kwa ujumla. Sambamba na hayo, Mhe Mhapa ametoa pongezi zake za dhati kwa Mhe. Serukamba kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwake.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa