MKUU WA MKOA IRINGA, AIFAGILIA IRINGA –DC
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa –DC)
Mkuu wa Mkoa Iringa Mh Ally Hapi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kupata Hati safi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Mh Hapi alisema hayo leo Mei 15 alipokuwa amehudhuria kikao Maalum cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikijadili hoja za mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ulioishia mwezi Juni mwaka 2019.
“kwa dhati naipongeza Halmashauri yenu ya Iringa kwa usimamizi mzuri katika miradi ya maendeleo na kusimamia ukusanyaji wa mapato ambapo hadi kufikia Aprili 20,Halmashauri hiyu ilikuwa imekusanya kiasi cha bilioni 2.6 sawa na asilimia 90 ya lengo la kukusanya bilioni kiasi cha milioni 306 ili kufikia au kuvuka lengo la bilioni 2.9 ifikapo mwezi Juni mwaka huu”alisema.
Aidha ameelekeza menejimenti ya Halmashuri ya Wilaya ya Iringa kufanya ufutiliaji wa kina ili kubaini kasoro katika mfumo ili kuhakikisha kunakuwa na taarifa sahihi na kuwalipa wakandarasi na wadau mbalimbali waliofanya kazi za Halmashauri kwa wakati ili wanufaike na stahiki zao.
“Naagiza mtafute fedha ili mlipe madeni yote yanayostahili kulipwa ili kuwawezesha wadai kunufaika na stahiki zao lakini pia kuwapa tenda Wazabuni wenye uwezo ili miradi yote inayotekelezwa imalizike kwa wakati”alisema.
“Hongereni sana, lakini pia hakikisheni mnatumia wazabuni wenye uwezo ili miradi ya maendeleo iwe na ubora unao stahili na iwe inaendana na kasi ya Serika”
Alimuagiza Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala kufuatilia madeni ya watumishi na kuwalipa na iwapo hakuna fedha atumie mtumishi wake na kuagiza pia, hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa watumishi wote ambao hawana weledi il kuinusuru Halmashauri kutowekewa hoja zisizokuwa za lazima.
Aidha Mh Hapi aliwaomba waheshimiwa madiwani kusaidia utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya Ugonjwa COVID 19,na kuwahamasisha dhidi ya uchukuaji wa Tahadhali ya maambukizi ya Ugonjwa huo lakini pia,amewataka wazingatie ushauri wa wataalam wa afya katika maeneo yao.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa