MH. QUEEN SENDIGA AISIFU WILAYA YA IRINGA KWA MAANDALIZI MAZURI YA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU AGASTI 1, 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Mhe. Queen Sendiga Julai 6 mwaka huu amefanya ziara ya kutembelea miradi na kukagua njia zitakazotumika wakati wa kuukimbiza mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokewa Agasti mosi katika Kata ya Migoli.
Wilaya ya Iringa utakimbiza mwenge huo katika katika Halmashauri zake mbili ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na kuukabidhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Agasti 2.
Mwenge wa Uhuru utapita na kukagua shamba la kilimo cha Korosholilipo Isimani, klabu ya ya mapambano dhidi ya rushwa shule ya Sekondari ya Mwalimu Nyerere, mradi wa maji, ujenzi wa barabara ya lami Kihesa, ukarabati wa miundombinu shule ya wasichana Iringa, ujenzi wa jengo la maabara hospitali ya Wilaya Frelimo pamoja na Ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kigungawe.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi.Happiness Seneda "Hongereni kwa maandalizi na niwatakie kila la heri katika katika hatua zilizobakia za maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa uhuru utakapofika" akiwa katika ziara hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh.Sendiga.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa