Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga ataika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuangalia ilipo jikwaa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Queen Cathbert Sendiga amewaasa Watumishi kufanya kazi kwa weledi ili kuleta maendeleo chanya ambayo ni chachu ya maendeleo.
Mh.Sendiga alisema hayo Juni 10 mwaka huu wakati alihudhuria mkutano maalum wa Baraza la Madiwani ambapo wajumbe watakuwa wakipia,kujadili na kutoa maoni katika taarifa ya majibu ya Menejimenti ya hoja zote za Ukaguzi wan Nje wa mwaka wa fedha 2019/2020.
“Kuwa na hati yenye mashaka isiwavunje moyo kwa sababu miaka yote wataalamu ni ninyi isipokuwa mrudi mjiulize ni wapi mmekosea ili kasoro hiyo isijirudie katika mwaka mwingine wa fedha lakini mzingatie maelekezo na maagizo mtakayokuwa mkipewa na wakaguzi wa nje”alisema Mh.Sendiga na kuongeza
“Baadhi ya hoja inajibika na hazina sababu ya kuendelea kuwepo katika orodha nah ii imesababishwa na baadhi yenu kushindwa kuwajibika kwa nafasi yake mfano haiwezekani mashine ya POS isitumike zaidiya 900 hii ni aina ingine ya kupoteza mapato ama uchepushaji wa fedha za serikali”alisema pia,
“Halmashauri ya Wilaya ya Iringa nimeambiwa imebarikiwa ardhi inayokubali mazao yote,serikali imekuja na mkakati wa kilimo cha Alizeti na ofisi yangu muda si mrefu itakuwa na mbegu za kusambaza na hii ni baada ya mimi na Katibu Tawala kwenda kumuona Waziri mwenye dhamana na kumuambia matamanio yetu na dhamiri yetu ya kutamani Mkoa wa Iringa nao ulime zao hili la Alizeti na Mh.Waziri
amekubali”alisema.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi.Hapiness Seneda amewakumbusha wakuu wa Idara kutimiza wajibu wao sambamba na kuwataka kuzipatia uvumbuzi changamoto za watumishi wa Idara zao waliopo katika ngazi za Msingi.
“Katika ziara yangu ya kuzungumza na Watumishi walikuwa na changamoto na kero nyingi ambazo Wakuu wa Idara mnaweza kuzipatia uvumbuzi nilitoa maelekezo na leo nakumbushia kuhusu suala hilo”alisema.
Pia,alikumbushia suala la kuwahi na kutekeleza majukumu ya kila siku kila mmoja katika eneo lake la kazi na kuagiza kwa Menejimenti kubuni vyazo vipya vya mapato ili kuwa na uhakika wa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa