Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa -DC)
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ya tekeleza utoaji wa mikopo kwa Wanawake,wenyeulemavu na vijana.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imetoa kiasi cha Shilingi milioni 78 zikiwemo Pikipiki mbili kwa Wanawake,Watu wenyeulemavu na Vijana katika kipindi cha robo ya kwanza yam waka wa fedha 2020/2021 .
Akizungumza kabla ya makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela amewasisitiza vijana hao kutumia vyombo hivyo kwa uangalifu ikiwemo kuvaa kofia na viatu vigumu ili kujikinga na ajali kwa kuwa bado wanahitajika katika Jamii zao na Taifa kwa ujumla.
Mh. Kasesela amesema utoaji wa mkopo huo wa pikipiki ni ombi la kijana Asajigwe ambaye ametoa kama wazo kwa kuwa vijana wengi hawatulii sehemu moja hivyo kwa kuwanunulia vitendea kazi inasaidia kuwaweka pamoja vijana hawa ambao wameamua kujiajili katika sekta ya usafirishaji.
Alisema suala la vijana kujiunga katika vikundi na kufanya shughuli za maendeleo ni suala la kupongezwa kwani linapelekea kupungua kwa wimbi la uharifu lakini pia kuwepo kwa ongezeko la ajira kwani wanaweza kulipa na kurudia kukopa mpaka wana kikundi wote kumi kumiliki chombo hiko.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw.Wapa Mpwehwe amesema huo ni muendelezo wa utoaji wa mikopo katika Halmashauri yake .
“zoezi hili la utoaji wa mikopo kwa Halmashauei yetu ni endelevu kwa kuwa kila mwaka tunatoa mikopo kwa vikundi vya wanawake,watu wenyeulemavu na vijana na katika robo hii ya mwaka wa fedha 2020/2021”alisema.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Bi.Saumu Kweka amesema katika awamu hii wanawake walipatia mkopo wa shilingi 42,vijana milioni 30 na watu wenye ulemavu milioni 6 ambapo katika milioni 30 za vijana milioni tano ndio zimenunua pikipiki mbili walizokabidhiwa vijana wa kikundi cha Mapambano.
“Hali ya changamoto sio mbaya sana ingawa kuna changamoto kwa vijana kwa kuwa waliowengi hawafanyi shughuli zao katika eneo moja wengi huama ama kuwanunulia vitendea kazi kutasaidia urudishaji wa mkopo mkopo huu”alisema Bi.Kweka
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa